Tumsifu Yesu Kristo ndugu zangu. Kwanza namshukuru MUNGU kwa kutujalia uzima mimi na wewe hata tukaweza tena kuiona siku hii ya leo. Kwa neema na baraka, MUNGU amenipa mawazo ya kutengeneza hii blogspot kwa lengo la kueneza Injili na kusaidiana katika kutafakari upendo wake na wa mwanae wa pekee Bwana wetu Yesu Kristo juu yetu sisi wanadamu. Tutatumia Biblia kama muongozo wetu huku tukimuomba Roho Mtakafifu atujalie upeo wa kutafakari na kuelewa upendo na huruma kuu ya MUNGU.
Hakuna mwanadamu aliye mkamilifu hivyo naomba tusaidiane mawazo, maoni na mapendekezo ili kuweza kueneza neno la MUNGU na kutenda yale yaliyo mema ili mwisho wa maisha yetu ya hapa duniani uwe wa matumaini na faraja.
Asante!
No comments:
Post a Comment