Wednesday, 27 February 2013

MUNGU ni Nani?


Wakolosai 1:16-17 "Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye" 

Baadhi ya sifa za MUNGU.

1. Hakuumbwa na pia ni wa milele. (Yohana 1:1-3 na Mwanzo 21:33)

2. Anaweza yote. (Luka 1:37)

3. Anajua yote. (Zaburi 147:5)

4. Yupo kila mahali. (Yeremia 23:23-24)

5. Mungu ni Roho. (Yohana 4:24)

6. Mungu ana nafsi tatu. MUNGU Baba, MUNGU Mwana, MUNGU Roho Mtakatifu. (Mathayo 3:16-17, Yohana 1:1-14, 14:9-20)

7. Hana mwisho. (Isaya 40:12-13)

8. Ni mwenye upendo. (Waefeso 2:1-7, 1Yohana 3:1, 1Yohana 4:9-10). Mungu HANA upendo, Mungu NI upendo.

9. Tabia yake ni tunda la Roho lililoelezewa katika Wagalatia 5:22-23.

10. Habadiliki. Hisia zake haziwi moto na baridi kama wanadamu.

(Waebrania 13:8). 

Upendo wa MUNGU kwa Wanadamu




Isaya 53:3-7 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.