Wednesday, 25 June 2014

AHADI 15 ZA ROZARI TAKATIFU

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.

1. Yeyote yule atakayesali kwa imani rozari hii takatifu atapokea neema kuu zenye nguvu

2. Naahidi ulinzi wa kipekee na neema za kipekee kwa yule atakayesali rozari hii

3. Rozari itakuwa silaha kubwa dhidi ya nguvu za kuzimu, itaharibu maovu, itapunguza dhambi na kushinda kutofautiana

4. Itafanya fadhila kukua, kazi nzuri kuongezeka, itapatia roho huruma tele toka kwa MUNGU, itaondoa hamu ya wanadamu kupenda mambo ya dunia na majivuno yake na kufanya wapende zaidi mambo ya mbinguni. Ooh, ni kwa namna gani roho hizo zitajifurahisha na kubarikiwa kwa namna hii.

5. Roho zitakazojikabidhi kwangu kwa njia ya kusali rozari, kamwe hazitapotea.

6.  Yeyote atakayesali rozari kwa uaminifu huku akiyatafakari matendo makuu  ya rozari, kamwe hatashindwa na ubaya. MUNGU hatamwadhibu katika hukumu yake, hatapotea katika kifo asichopangiwa na atabaki katika neema za MUNGU na kustahili kupata uzima wa milele.

7. Yeyote atakayekuwa mwaminifu katika kusali rozari, kamwe hatakufa bila ya kupokea Sakramenti takatifu za Kanisa.

8. Wote watakaokuwa waaminifu katika kusali rozari watadumu katika mwanga wa MUNGU katika maisha yao na saa yao ya kufa na kupata neema zake tele; katika saa yao ya kufa watashiriki fadhila za watakatifu waliopo peponi

9. Nitawatoa toharani wale wote waliokuwa waaminifu katika kusali rozari

10. Watoto wangu waaminifu katika kusali rozari watapata fadhila kuu ya utukufu Mbinguni.

11. Utapata yale yote unayoniomba kwa kusali rozari

12. Wote wale wanaoeneza rozari hii takatifu nitawasaidia katika mahitaji yao

13. Nimepata toka kwa mwanangu Mtukufu kuwa mawakili wote wa rozari takatifu watapata
waombezi toka baraza lote kuu la Mbinguni wakati wa maisha yao na wakati wa saa yao ya kufa.

14. Wote wanaosali rozari hii takatifu ni wanangu, na kaka na dada wa mwanangu wa pekee YESU KRISTO

15. Ibada kwa rozari takatifu ni ishara kuu ya kuelekea ukombozi

65 comments:

  1. AMINA.asante sana jamen nabarikiwa kuzisoma ahadi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aise aminasana nabarikiwa sana kwanjia ya Mama Maria

      Delete
    2. Mungu awabariki kwa kazi mnazofanya.Asanten sana nabarikiwa.

      Delete
  2. Naomba nitumiwe zaidi habari za kiroho katika email yangu kwani nafarijika mno

    ReplyDelete
  3. Amina, asanteni sana,nabarikiwa kwa Imani nikisoma ahadi.zidi kutupasha habaro za kiroho kwa email yangu

    ReplyDelete
  4. Nimewapata vizur sana, mungu ni mwema

    ReplyDelete
  5. Asante Sana Mama Maria awaongoze ili watu wengi zaidi wapate faida ya ahadi hizi za rozari takatifu. Mimi nimefarijika mno



    ReplyDelete
  6. Naomba baraka zako Mamaa yetu wa msaada wa daima. Uiombeee ulimwengu huu.

    ReplyDelete
  7. Asante mama wa rosary takatifu. Tunyenyekeee kwake hasa mwezi huu was kumi tutako uanza kesho.

    ReplyDelete
  8. Asanteni kwa mafundisho mazuri Ya usuyo mama yetu Bikira Maria na Ahadi za rozari takatifu. Nimebarikiwa sana.mnisaidie mengi kupitia whatsapp Namba yangu +258842330967

    ReplyDelete
  9. Ninabarikiwa Sana na habari za mama Maria kwani amenitendea Mambo makuu na anaendelea kunitendea.naomba niendelee kupokea mengi kuhusu mama yetu.nafarijika mnoo.

    ReplyDelete
  10. Ubarikiwe Sana tuombe amani na upendo kwa Mama Maria

    ReplyDelete
  11. AMINA 🙏🙏🙏...KWANI NI RAHA ILIYOJE KUSALI ROZARI TAKATIFU YA MAMA YETU BIKIRA MARIA ALIYE KINGIWA DHAMBI YA ASILI.

    ReplyDelete
  12. Amina mama yetu mwenye huruma Uzidi Kutuombea.

    ReplyDelete
  13. Asante Mama wa Rozari Takatifu "ni kweli unatimiza ahadi hizi". Naomba neema ya kudumu katika Sala ya Rozari.

    "Mimi ni Mali Yako eee Maria, Malkia Wangu na Mama Yangu na Yote Niliyonayo ni Mali Yako". - Ahadi ya Mlegio Maria.

    ReplyDelete
  14. Mama Maria asante sana mama kwa upendo wa pekee

    ReplyDelete
  15. Hail Mary mother of God, Pray for us sinner now and the hour of our death.
    Amen

    ReplyDelete
  16. Amina Mungu ni pendo na uzima wa kweli

    ReplyDelete
  17. Asante Mama wa rozari takatifu naomba unitumie novena ya bikira Maria kwenye Email yangu

    ReplyDelete
  18. Amen,may the true power of God take control.

    ReplyDelete
  19. MUNGU ni mwemaa Sana,nmebarikiwa mno

    ReplyDelete
  20. Amani na salama katieti

    ReplyDelete
  21. Amina nimebarikiwa

    ReplyDelete
  22. Asante sana
    nahitaji kujiumga naglupu lenu

    ReplyDelete
  23. Nimebarikiwa sana kuona ahadi hizi za rosari takatifu 🙏🏾❤️

    ReplyDelete
  24. Nimebarikiwa kusoma ahadi hiz naomba kuona zaidi katika email yangu

    ReplyDelete
  25. Ahsante Sana Mama Kwa ahadi zako adilifu. Utuombee sisi na Dunia nzima

    ReplyDelete
  26. Amina sana nabarikiwa katika kubadilisha maisha yangu kupitia Rozari takatifu ya Mama

    ReplyDelete
  27. Amina mama mtakatifu ni funze zaidi rozali

    ReplyDelete
  28. Asanteni sana

    ReplyDelete
  29. Mama na wanae tunakimbilia ulinzi wako...

    ReplyDelete
  30. Thank u mother mary..thank u mlio tanga ahadi hzi..❤ catholic 4ever

    ReplyDelete