Wednesday, 25 June 2014

ROZARI YA HURUMA KUU YA MUNGU

 Mtakatifu Maria Faustina

 HISTORIA

Sista Faustina alizaliwa tarehe 25 August 1905 katika kijiji cha Glogowieko nchini Poland, na jina lake la ubatizo lilikuwa Helena.
Akiwa na umri wa kiaka 20, Bwana alimwongoza kuingia katika utawa wa shirika la Mama wa Huruma ambako (kama kawaida) alibadilisha jina na kuitwa Sista Maria Faustina, akaweka nadhiri za kwanza mwaka 1928.

MATUKIO
Bwana Yesu alianza kumtokea Sista Faustina mfululizo tangu mwaka 1930 hadi 1938. Alimtokea ili kumwandaa kwa ujumbe mkubwa wa maisha wa kuitgazia dunia nzima ibada ya Huruma ya Mungu, ambayo ilikuwa na madhumuni yafuatayo;
  1. Kuandaa ujio wa Pili wa Bwana wetu Yesu Kristo aliye Mfalme wa Huruma.
  2. Kuokoa roho zilizoko Toharani.
  3. Kuwaongoa wakosefu ambao wameshapoteza neema ya kujiombea.
  4. Kuitangaza Huruma ya Mungu.
Tarehe 22 Februari 1931 alipokuwa na umri wa miaka 26, Sista Faustina alitokewa kwa mara ya kwanza na Bwana Yesu na kumchagua kuwa mjumbe wa Ibada ya Huruma ya Mungu. Sista Faustina anatueleza:
  


"Jioni, ndani ya chumba changu, huku nikiwa nimepiga magoti kwa woga na furaha, nilimuona Bwana Yesu akiwa amevaa vazi refu jeupe. Aliinua mkono juu kwa kubariki, na mkono mwingine ulishika nguo yake kifuani. Kutoka ndani ya nguo kifuani kulitokea miale ya aina mbili ya mwanga inayong'ara. Miale ya upande wa kulia ilikuwa myekundu na miale ya upande wa kushoto ilikua myeupe" 

YESU NINAKUTUMAINIA

"Mchoro halisi wa Huruma Kuu, uliochorwa chini ya usimamizi wa Sista Faustina"

Sista Faustina hakujua maana ya aina hizo mbili za miale ya mwanga aliyoiona, na siku moja alimuuliza Bwana Yesu maana yake. Bwana Yesu kwa utulivu mkubwa alimwambia, "Miale miwili hiyo ya mwanga inayotoka ndani ya moyo wangu ni alama ya Damu na Maji yaliyomwagika kutoka katika Moyo wangu wenye Huruma, siku ile nilipojitoa sadaka Kalvarini. 
Miale Myeupe ni alama ya Maji yanayoosha roho na miale Myekundu ni alama ya Damu inayoleta uzima wa Roho za watu. Miale hii inalinda Roho kabla ya adhabu ya Baba yangu: Kwa anayeishi katika ulinzi wake (Miale hiyo), mkono wa Hasira ya Mungu hautamfikia kamwe.

Kisha Bwana Yesu alimfundisha Sista Faustina sala hii: "Ee Damu na Maji vinavyotoka katika Moyo Mtakatifu wa Yesu, kama chanzo cha Huruma yake, ninakutumaini"

Bwana Yesu huku akimwonyesha Moyo wake Mtakatifu alimwambia Sista Faustina "Chora picha kama unavyoona, na  uandike YESU NINAKUTUMAINIA. Mimi ni Mfalme wa Huruma.
Ninatamani picha hii iwekwe na kuheshimiwa kwanza Kanisani kwako na baadaye Ulimwenguni kote. Naahidi ushindi kwake na maadui zake walio Duniani na hasa saa ya kufa kwake. Mimi mwenyewe nitamlinda. Kwa njia ya picha hii nitatoa neema nyingi kwa watu watakaoitunza vizuri, hata kwa wale watakaoitazama"

6 comments:

  1. Web site hii ni nzuri sana ningeshauri juhudi zifanyike kutafsiri sala ambazo zipo kwenye website ya Laudate toka Rome kwani ina sala nyingi sana ambazo tunazihitaji. Pili nitumie sala ya toba inayosaliwa baada ya sala ya Rozari ya Huruma baada ya Litania.yake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndunguru kama umetumiwa sala ya toba naomba na mie unitumie

      Delete
    2. ndunguru kama umetumiwa sala ya toba naomba na mie unitumie

      Delete
    3. Sala ya Kuwaombea wengine Huruma ya Mungu unaweza kuipata kupitia Radio Maria muda wa saa 9.00 jioni.

      Delete
  2. Nimefurahi sana kupata historia hii,imenitamanisha mno,naomba tu Mungu anikamilishe katika upendo na hekima

    ReplyDelete
  3. naipenda sana hstoria hii kwani inanikumbusha uwepo wa Mungu Mwana katika ishara zake alizozitoa na kutufafanulia kwa kupitia Mt.Sr.Faustina

    ReplyDelete