Saturday, 21 June 2014

MATENDO YA ROZARI

Rozari imegawanyika katika matendo yafuatayo:
Matendo ya FURAHA, UCHUNGU na UTUKUFU.
Na mnamo October 16, 2002 baba mtakatifu marehemu John Paul II aliongeza matendo mengine ambayo yaliitwa matendo ya MWANGA.

MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)

Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu  atujalie unyenyekevu.
Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.

MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)

Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.

MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)

Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.

MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.

65 comments:

  1. Mama Bikira Maria utuombee sisi wakosefu sasa na saa kufa kwetu amina.

    ReplyDelete
  2. Bikira maria mama wa mkombozi utuombee sisi wakosefu

    ReplyDelete
  3. Bikira maria mama wa mkombozi utuombee daima mama yetu mpendwa.

    ReplyDelete
  4. Amen, nakaribisha maoni, sala, shuhuda na mapendekezo yoyote uliyonayo ili tuweze kueneza neno la MUNGU.Nitumie kwa robert.j.kimaro@gmail.com

    ReplyDelete
  5. Bikira Maria utuombee kwa mungu, tusamehewe dhambi zetu hasa kipindi hiki cha Mwezi wa rozari takatifu...

    ReplyDelete
  6. Nifanyaje ili nami niweze kushiriki japo tendo moja la Rozari Takatifu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Muombe Mungu, naye atakusaidia kushiriki, si tu tendo moja, bali matendo yote matano kwa siku.

      Mungu awe nawe na aendelee kukubariki. Amina.

      Delete
  7. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  8. Bikira maria utuombee Kwa mungu sisi wakosefu wakati huu wa mfungo

    ReplyDelete
  9. tumsifu yesu kristo, nilikuwa na wazo kama itawezekana haya matendo yawekwe kwenye mfumo wa pdf ili iwe rahisi pia kwa mtu kuya download na kuwa nayo kwenye kifaa chake kama simu au komputa endapo atahitaji kusali bila kuwa na internet connection kwenye kifaa chake

    ReplyDelete
  10. Kristu, Tumaini letu, Tumaini letu Kristu. Kabisa wazo la kuweka matendo katika mfumo wa pdf itakuwa vizuri zaidi naomba sana ufikirie hilo wazo

    ReplyDelete
  11. Bikira Maria mama wa huruma.Utuombee sisi wakosefu

    ReplyDelete
  12. Bikira Maria Mama wa Huruma tusaidie nasi tufike katika ufalme wa Mungu.

    ReplyDelete
  13. Tumsifu yesu Kristu wapendwa. Mwenyezi Mungu awalinde daima na Milele Amina.

    ReplyDelete
  14. Mungu ni mwema daima

    ReplyDelete
  15. bikira maria mama wa msaada utuombe

    ReplyDelete
  16. Tumsifu Yesu Kristo Milele na Milele Amina mama Bikira Maria Tuoembee sisi na utukinge Maovu

    ReplyDelete
  17. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  18. Tumsifu Yesu Kristo milele na milele,Amina.
    Bikira Maria Mama wa Mungu tuombee tuweze kushinda majaribio. Tuongozwe na mwanga wa Kristo katika maisha yetu ya kila siku. Amina.

    ReplyDelete
  19. Rosari ni sala yenye nguvu sana. Bikira Maria amepewa nafasi ya pekee sana na Mungu. Tusali rozari kila siku hakika tutaonja upendo,tutapata msaada na huruma ya Mungu. Shuhuda ziko nyingi hata leo. Nakumbuka tokeo la mama huyu kwangu mwenyewe october 1991 wilayani Kahama.Ilikuwa ni baada ya kusali rosali mfululizo kwa muda wa miezi 3, nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi.Ilikuwa usiku wa saa tano hivi nikiwa nimejipumzisha kitandani baada kujisomea kidogo.Ghafla ndani kukawa mwanga mkali, nikafikiri ninaota,nikakaa, mwanamke mwenye vazi jeupe mpaka chini akaingia akaja mpaka pale kitandani akiwa ameshikilia rozari, akasimama kama dk5 ameniangalia kisha akatoweka bila kusema neno.Nilijiliuliza sana nimeona nini,baadae ndo zikaja fahamu ya kuwa yule alikuwa ni Mama. Mpaka leo huwa natamani kuweka kitu cha kumbukumbu eneo hilo ambalo kile kijumba kidogo cha nyasi kilishabomoka. Sijajua niweke nini hasa kwa heshima ya mama!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bikira maria mama wa miujiza ...anatenda amenutendea mema mengi sana yasiyofikirika ...blessed are you among women ...thanks you mama

      Delete
    2. Mama wa Mungu, malkia wa amani. Ni kweli ukisali rozari utajisikia amani n hali fulani ya utulivu moyoni. asante kwa ushuhuda wako ndg

      Delete
    3. Hongera Sana usiache kusali Rozari hata mm naitamani nimuone.pale alipotokea weka sanamu ya Bikira Maria

      Delete
    4. Nini maana ya Sapuli

      Delete
    5. Nini faida za sapuli

      Delete
  20. Bikira Maria mama wa huruma utuombee Sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. Amina

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bikira Maria mama wa huruma utuhurumie na kutusaidia Katika matatizo mbalimbali tunakutana nayo

      Delete
  21. Tumsifu yesu kristo..asante Kwa matendo ya rosary maana nilikua nimeyasahau ubarikiwe sana.

    ReplyDelete
  22. AMINA ....ROZARI TAKATIFU NI NJIA YA KUFIKIA KWA BABA

    ReplyDelete
  23. Thanks be to the almighty Fatherlord JESUS CHRIST

    ReplyDelete
  24. Bikira maria mama wa msaada utuombe na kutusikiliza

    ReplyDelete
  25. Bikira mwenye moyo safi- utuombee

    ReplyDelete
  26. Holy Mary mother of God, pray for us Sinners

    ReplyDelete
  27. Utuombee mzazi mtakatifu wa Mungu tujaliwe ahadi za kristo

    ReplyDelete
  28. Holy Mary mother of God, Pray for us

    ReplyDelete
  29. Mama mwenye huruma utukumbuke sisi wakosefu

    ReplyDelete
  30. Bikira Maria mama mwenye huruma utuombee

    ReplyDelete
  31. Bikira Maria salama ya wagonjwa utuombee

    ReplyDelete
  32. Bikira Maria mkingiwa dhambi ya asili utuombee

    ReplyDelete
  33. Bikira Maria kipawa cha hekima utuombee

    ReplyDelete
  34. upendo wa mama kwa watoto wake. mama huyu anatupenda hakika. ujumbe wake kwa wale aliowatokea ni toba, kusali na kuwaombea wengine. Mama hataki watoto wake wapotee. Mama wa Mungu wewe n mwalimu wetu. nifundishe namna ya kukupenda na kumfuata mwanao. na saa ya kufa kwangu uje na mwanao Yesu uniongoze mbinguni.

    ReplyDelete
  35. Namusifu yesu christu kwa kutukomboa katika utumwa wa shetani utukufu wake izidi milele na milele anmina

    ReplyDelete
  36. Upendo wa mama ju yetu u mwingi sikuzote hata milele

    ReplyDelete
  37. Wapendwa kweli Mama Maria anatuombea sana Kwa Mwanae Yesu Kristo.
    Ninawasihi sasa tunapoandika majina haya tuyaandike Kwa heshima maana hata jina la mtu halianzi kwa herufi ndogo.

    Ukiandika yesu ni tofauti kubwa sana na Yesu. Ukiandika mungu ni tofauti kubwa sana na Mungu. Wanaonielewa ninaomba wachanganue haya majina.

    ReplyDelete
  38. Kioo cha haki utuombee
    Sababu ya furaha yetu utuombee
    Kikao cha hekima utuombee

    ReplyDelete
  39. Bikira Maria msaada wa saima utuombee🙏

    ReplyDelete
  40. Pray for us o holy mother of God, that we may be made worth of the promises of Christ.

    ReplyDelete
  41. Mama Bikira maria mtetezi wa wanyonge utuombee

    ReplyDelete
  42. Ee Bikira Maria, naomb ukayaongoze maish yang, masomo yang na familia yang kwa ili tukumbuke kuw kimbilio let lipo kwak peke yang

    ReplyDelete
  43. nechamabula@gmail.com

    ReplyDelete
  44. salamu Maria ni sala inayo vunja na kuharibu nguvu za giza inapo saliwa mara nyingi, kwa sababu mchakato wa utekelezaji wa agano jipya ambalo Mungu alifanya na wanadamu pitia mwanae bwana wetu Yesu kristu ili kutukomboa na kutuweka huru na nguvu za giza ulianza kwa maneno haya matakatifu, "salamu uliye pewa neema bwana yu nawe", yaliyo nenwa na Malaika Gabriel siku ya kupashwa habari bikira Maria Luka 1:28, kwa hiyo tunavotamka mara nyingi maneno haya tuna huisha ndani yetu agano hilo la Mungu na wanadamu na kwa sababu agano hilo lili muweka shetani chini ya Miguu yetu Hivyo tuki sali salamu Maria mara nyingi shetani huchanganyikiwa kwakua tuna mkumbusha mara nyingi kushindwa kwake na kuutangaza ushindi wa bwana wetu Yesu kristu katika agano jipya. Salamu Maria ni sala yetu ya ushindi dhidi ya nguvu za giza na ibilisi, tuisali mara nyingi katika rozari takatifu. TUMSIFU YESU KRISTU.....

    ReplyDelete
  45. Mama bikira Maria usiye na doa utuombee kwa mwanao Mpenzi Yesu kristu

    ReplyDelete
  46. Ee mungu mwenyezi wa milele utuokoe siku zote za maisha yetu,maana bila wewe hatuwezi kitu, tunajiweka mikononi mwako kwa njia ya kristo bwana wetu AMINA🙏🙏🙏

    ReplyDelete
  47. Bikira Maria mama wa msaada, utuombee na utusahidie🙏🏾

    ReplyDelete
  48. Mungu mwema kwa wote

    ReplyDelete
  49. Nihaki ya mkisto kuisari rosary ya mama maria kwani ndio maombi ya kwanza

    ReplyDelete
  50. Mama utuombee

    ReplyDelete
  51. macklina zacharia

    ReplyDelete
  52. Bikira maria Mama wa wakosefu ,UTUOMBEE🙏

    ReplyDelete
  53. Bikira Maria mama wa yatima...Utuombee

    ReplyDelete
  54. Mama bikira Maria msaada wa daima utuombee

    ReplyDelete
  55. Maria tuombeee

    ReplyDelete