Neno Rozari limetokana na neno la Kilatini "Rosarium" lenye maana ya Taji la Mawaridi.
Mama yetu Bikira Maria aliwafahamisha baadhi ya watu aliowatokea kua kila mara mtu anaposali sala ya "Salamu Maria" anampa mama Maria waridi na hivyo kila anayesali rozari nzima humkabidhi mama Maria taji la mawaridi.
Rozari takatifu hujulikana kama sala kamili kwa sababu ndani yake hupatikana hadithi kamili ya ukombozi wetu sisi wanadamu.
Katika rozari tunatafakari matendo ya Furaha, Uchungu na Utukufu ambayo yanaelezea historia nzima ya maisha ya Bwana wetu YESU KRISTO na ukombozi uliopatikana katika yeye kwetu sisi wanadamu.
Katika sala ya Salamu Maria tunamkaribisha mama Maria atuombee sisi wanadamu kwa mwanawe bwana wetu YESU KRISTO hivyo kufanya sala zetu kuwa na nguvu zaidi mbele zake MUNGU.
YESU hawezi kukataa maombi ya mama yake na hivyo ni wajibu wetu kufanya bidii katika kusali rozari takatifu ya Mama yetu Bikira Maria.
Dhumuni kuu la kusali rozari ni kwa ajili ya kuwaombea wakosefu waongoke na kumrudia MUNGU katika KRISTO YESU mwanawe wa pekee aliyetukomboa dhidi ya yule muovu kwa mateso, kifo na ufufuko wake. Kila mara mtu au watu wanapopiga magoti na kusali rozari mama Bikira Maria huja haraka na kukaa pembeni yake/yao wanaosali na kusali nao, na haji peke yake kwa kuwa yeye ni Mama wa MUNGU na Malkia wa Malaika huja na jeshi kubwa la Malaika. Na kwa kuwa yeye ni mama wa YESU, hivyo YESU huja nae pia na YESU ni nafsi ya pili ya MUNGU hivyo MUNGU BABA na MUNGU ROHO MTAKATIFU huja pia kwa sababu hawatengani kamwe.
http://www.theholyrosary.org/
AMINA...MUNGU ANATUPENDA SANA PAMOJA NA MAMA YETU BIKIRA MARIA
ReplyDeletemungu ni mwema
ReplyDeleteKila wakati
DeleteTumsifu yesu kritu
ReplyDeletegod is good
ReplyDelete