Ukurasa 11, Kitabu - Mawaridi Ya Sala
Baba wa milele, ninakutolea Moyo Mtakatifu wa Yesu, na Upendo wake wote, na Mateso yake yote, na Mastahili yake yote.
Kwanza.
Kulipia dhambi nilizozitenda leo na wakati wa maisha yangu yote. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote na milele, Amina.
Pili.
Kuyatakasa mema niliyoyafanya le na wakati wa maisha yangu yote. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote na milele, Amina.
Tatu.
Kutolea mazuri niliyopaswa kufanya na yale ambayo leo sikuyafanya na wakati wa maisha yangu yote. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote na milele, Amina.
"Mtawa wa Maklara aliyekuwa amekufa, alimtokea mkuu wake mara, aliyekuwa akimuombea, akamwambia "nilienda Mbinguni kwa sababu ya sala hii, kwa kusali kila siku nililipa madeni yangu"
(HII SALA SIYO BADALA YA KITUBIO)
No comments:
Post a Comment