Ukurasa - 12, Kitabu- Mawaridi ya Sala
Bwana wetu YESU KRISTO alimwambia Mt. Getrude Mkuu kwamba kila isaliwapo sala hii roho 1,000 hufunguliwa Toharani.
Sala hii pia inawahusu wakosefu wa hapa duniani nayo huwalipia madeni yao ya wakati wa maisha yao.
"Baba wa Milele ninakutolea damu ya thamani kuu ya Yesu mwanao Mungu, nikiunganisha na sadaka ya misa takatifu inayoadhimishwa leo popote duniani, kwa ajili ya roho zote zilizomo toharani, kwa ajili ya wakosefu wote duniani, kwa ajili ya wakatoliki walio wakosefu, kwa ajili ya wakosefu wa nyumbani kwangu mwenyewe, na wale wa familia yangu"
Amina.
Mt. Getrude Mkuu alizaliwa Ujerumani mwaka 1263. Alikuwa mtawa Mbenedikini na alitafakari mateso ya Yesu ambayo yalimfanya kulia kila mara. Alifanya malipizi mengi na alitokewa na Yesu mara nyingi. Alifariki tarehe 16 Nov. 1334, siku ambayo ni sikukuu yake.
No comments:
Post a Comment